Chris Brown aongezewa siku zingine 131 za kukaa jela
Mwanamuziki wa Marekani Chris Brown atasalia jela kwa siku nyingine 131 baada ya kukiri kukiuka amri ya mahakama kuhusu kifungo cha nje alichokuwa amepewa na mahakama. Muimbaji huyo wa muziki wa mtindo wa R&B alikiri mahakamani mjini Los Angeles mnamo siku ya Ijumaa kuwa alitenda uhalifu mjini Washington Oktoba mwaka jana. Jaji alimuhukumu kifungo cha siku 365 jela ingawa alimpongeza kwa kuhudumia...